Jumatano, 18 Mei 2016

RAIS MUSEVENI AMPANDISHA CHEO MWANAE JESHINI

                                       Rais wa Uganda,Yoweri Kaguta Museveni,amempandisha cheo mwanae  Brigedia Kamerugaba Muhoozi, hatua ambayo inamfanya Brigedia Kamerugaba kufikia ngazi ya Meja Jeneral.Taarifa zaidi imeeleza kwamba kwa sasa mtoto huyo wa Museveni anakiongoza kikosi cha ulinzi wa Rais,(Special Force Command)
       Taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa mtoto huyo zina mnukuu akisema siku moja angependa kujihusisha na siasa.Taarifa hizo zinakuja na uvumi kuwa Rais Museven anamuandaa  wanaye ili aje kurithi mikoba ya Urais wa Uganda pale atakapo staafu.
                                           Rais Museveni ambaye ameiongoza Uganda kwa takribani miaka thelathini bila kutoka madarakani amekuwa akishushiwa lawama na watu mbalimbali kwa kuwapa vyeo vikubwa watoto wake pamoja na ndugu na jamaa akiwemo mkewe ambaye ni waziri katika serikali ya Rais Museveni 

 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni