Jumanne, 17 Mei 2016

HARUSI ZILIZOWEKA GUMZO MITAANI

        Mwana ASILI ASILIA leo napenda kukuletea matukio tofauti tofauti yaliyotokea katika uwanja wa harusi mbalimbali katika mitaa yetu.Harusi ni kitu cha pekee na mara nyingi kila mtu hutaka ya kwake ipendeze na kuvutia kuliko ya mwenzake na  hapo ndipo huweka vitu vya kibunifu na vya kuvutia. Twende pamoja polepole ,jicho kwa jicho tutizame ubunifu katika ndoa hizo;

         1.MABUSU YA AINA YAKE....
       Inafurahisha sana natamani ungekuwepo ushuhudie mwenyewe. hii ni ndoa iliyokuwa ya pekee sana , kwanza kabisa ilipambwa na wavulana pamoja na wasichana waliovalia mavazi ya kupendeza kwelikweli, lakini kilichokonga nyoyo za watu ni pale ulipofika wakati wa kupiga picha.
                               HAHAHA....Ilipendeza sana ,basi wale wavulana nawasichana waliwabeba maharusi kisha kama wanawagonganisha vichwa waliwasogeza taratibu na kisha vichwa vilivyokaribiana maharusi kwa hisia walijiachia na mabusu motomoto na kisha picha zikachukua nafasi.ilipendeza sana.

          2.WAKE WATATU MUME MMOJA. . . 
                                         
         Kama hujawahi shuhudi basi unapitwa na mengi.Imezoeleka kuona mwanamume akioa wake zaidi ya mmoja kwa wenzetu waislamu, cha kushangaza ni kwamb bwana asiliasilia ilimshuhudia bwana mmoja akifunga ndoa na wanawake watatu kanisani . . . .(ajabu kweli kweli). . Inasemekana kwamba wanawake hao waliridhia kwa hiari yao wenyewe kuolewa na bwana mmoja. CHEZEA KUPENDA WEWE. . .  

          3.KEKI YA KIPEKEE. . . 
        Katika harusi zote nilizowahi alikwa nimeona keki za kila aina ,kuna za duara ,za ngazi tano au sita na kadhalika, lakini keki niyoishuhudia katika sherehe ya juzi ilivunja rekodi ya keki zote nilizowahi ona.Watu bwana wabunifu achaa. . . Ilitengenezwa maridadi kwa umbo la bibi harusi vilevile ,yaani ukiangalia keki na ukamwangalia bibi harusi hakuna tofauti,kuanzia rangi,umbo, mavazi,na hata mtindo wa nywele . . . yaaan dah. . .! 
                                    




           4.BAJAJI  YABEBA MAHARUSI. . .
      Huenda huu ukawa ni ugunduzi mwingine wa jinsi ya kutumia bajaji. Katika harusi nyingi watu hujikoki kwa kwa kukodi magari ya kifahari kama Benz,Range na hata Humer,lakini kwenye harusi hii ilikuwa tofauti kwani maharusi walitumia bajaji kama gari lao maalumu.
                                      Bajaji hiyo ilipambwa vizuri kwa ajili ya kbebea maharusi .Usiidharau bajaji aisee. . . 

          5.HARUSI YA MAKANDARASI. . .
          HAHAHA. . . .Unaambiwa ukistaajabu ya Musa utayaona ya Filauni. Ni moja ya harusi zilizowaacha watu vinywa wazi,iliwahusisha wafanyakazi wa kampuni moja ya ujenzi wa barabara,ambapo ili kuudhihirishia umma kuwa wao ni wakandarasi waliamua kutumia katapila kama gari la maharusi. si hivyo tu bali kulikuwa na makatapila mengine yakifuata kwanyuma na kutengeneza msururu wa makatapila yaliyo pambwa vizuri. 
                                        Bwana na bibi harusi wao waliketi mbele kabisa kwenye kijiko wakiwa na myamvuli ya kukinga jua.Kwa raha zao jamani. . . .      

         

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni