Jumatatu, 16 Mei 2016

RAIS MAGUFULI , AVUNJA BODI YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA)


                                         
        Rais wa Tanzania John Magufuli amevunja bodi ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA).Hatua hiyo imeenda sambamba na kumsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wamamlaka hiyo Dkt,Ally Yahaya Simba .
        Taarifa iliyotufikia imesema kwamba Bw, Simba amesimamishwa kazi kwa sababu za kutosimamia ipasavyo mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS).
           "Nataka tukusanye mapato yote ya serikari yanayostahili na sitasita kuchukua hatua dhidi ya yeyote atakayekwamisha jambo hili," Amesema Rais Magufuli.

         Aidha bodi ya TCRA imekuwa ikiongozwa na  Prof, Haji Semboja. Taarifa hiyo imesema hatua hiyo ilisababisha Tanzania kupoteza mapato ya takribani Sh. bilioni 400 kwa mwaka.
          Mamlaka ya mawasiliano nchini  (TCRA) iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji,uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu  machi. 22. 2013
                     Kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na udhibiti wa mapato ya simu za ndani (offnet),kwa mujibu wa serikali.
          Rais amemuagiza waziri wa ujenzi,mawasiliano na uchukuzi Prof,Mbarawa,kumteua kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka hayo mara moja. Aidha amewataka waziri Prof,Mbarawa,katibu mkuu na naibu katibu mkuu katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya simu kwa simu za ndani (offnet) uanze kufanya kazi na nchi ipate mapato yanayostahili kukusanywa              
        "Nataka tukusanye mapato yote ya serikali yanayostahili na sitasita kuchukua hatua dhidi ya yeyote atakayekwamisha jambo hili." Amesema rais Magufuli.




Maoni 1 :

  1. Lucky Club: Slots, Table Games, Live Casino
    Lucky Club is a Swedish gambling operator that is luckyclub licensed and regulated by the Malta Gaming Authority. All games are powered by Microgaming, an industry leader

    JibuFuta