Jumamosi, 7 Mei 2016

UBINADAMU KAZI


         Baba mmoja alisafiri na mwanae wakiwa na punda mmoja.
Yule mzee akamweka mwanae juu ya punda yeye akatembea kwa miguu, WATU wakasema. "angalia anavyomdekeza mtoto!"
        Yule mzee akamshusha mtoto akapanda yeye WATU wakasema. "jamaa katili yeye amepanda juu ya punda mtoto anatembea!"
        Akaamua wapande wote wawili' WATU hao hao wakasema, huu unyanyasaji wa wanyama!" Wakashuka wakawa wanatembea kwa miguu. WATU tena wakasema washamba hawawezi kumtumia punda. FAHAMU hao ndio BINADAMU. Lolote utakalofanya watu watasema tu liwe zuri au baya, ishi uwezavyo usiangalie watu utakosa mwelekeo, mwangalie MUNGU asiye kigeugeu.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni