Uchongaji wa vinyago ni moja ya tamaduni bunifu za mwafrika .Utamaduni huo ambao chimbuko lake ni afrika mashariki hususani Tanzania hasa katika kabila la WAMAKONDE .Wamakonde hutumia magogo ya miti ya MPINGO ambayo huchongwa kwa ustadi mkubwa na umakini maridadi.Kwa kutumia zana kama ,nyundo,tindo nakadhalika, wachongaji hubuni maumbo mbalimbali kama vile maumbo ya wanyama mathalani twiga ,simba faru,na hata tembo,pia huweza kuumba maumbo ya binadamu hasa wamasai katika mavazi yao .Hali kadhalika maumbo ya nyumba, ramani na vifaa vya michezo kwa watoto.Ubunifu huu umekuwa ukiwaingizia kipato pale wanapouza vitu walivyobuni
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni