Maisha ya mwanadamu siku zote yamekuwa ya mapambano .Lazima mtu apambane darasani na hata maishani ili kuhakikisha anayasongesha maisha kwa siku zijazo.Hali hiyo haina tofauti na maisha ya wanyama ndani ya mbuga zetu za wanyama. .Wanyama huishi kwa kupambana pia, wale wababe kama simba ,duma ,chui na kadhalika hutu mia mabavu kuwanyanyasa wanyonge. Huwavizia wawapo malishoni na kuwashambulia.Lakini uonevu huo haufanikiwi kirahisi kwani wanyonge pia wana haki hivyo hujaribu kila linalowezekana kaujitetea .Katika harakati za kujitetea wanyama hao wakiwamo pundamilia,swala na kadhalika hutumia pembe zao pamoja na kwato kujinasua kutoka mikononi mwa maadui.Ni katika mapambano ndipo mshindi hupatikana. Mnyonge akishinda hukimbia , akishiwa basi hugeuka kitoweo cha adui hali kadhalika adui akishiwa kuondoka na majeraha mwilini ingawa ni nadra sana adui kushindwa."Maisha ni mapambano, TUPAMBANE"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni