Aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema akiungwa mkono na UKAWA (Umoja wa katiba ya wananchi ) ndugu Edward Lowassa ameanza ziara ya kutembea nchi nzima kwa lengo la kutoa shukrani kwa wananchi kwa ushirikiano waliouonyesha katika uchaguzi mkuu uliopita.
MH; Edward Lowassa akiwasalimu wananchi katika moja ya kampeni zake.
Kutoa shukrani si jambo baya lakini tukilitazama jambo hili kwa kina ,hasa tukiangaza jinsi litakavyofanyika ni dhahili litaghalimu kiasi kikubwa cha fedha . Zoezi hiyo pia litahusisha baadhi ya viongozi wa chama hicho jambo ambalo pia litazidi kuongeza gharama. Ina fahamika kuwa Lowassa ana uwezo kifedha na hivyo kugharamikia gharama hizo si tatizo,mbali na yeye pia chama nacho kina uwezo ,lakini kwa mtazamo wangu ni kama watakuwa wanafanya jambo la kitoto kwani kuna njia nyingi za mawasiliano ambazo zinaweza tumika na kufikisha ujumbe wa shukrani kwa walengwa haraka na kwa gharama nafuu mfano redio ,kwa njia ya luninga nk .Kama viongozi wenye nia ya kweli ya kuwaletea mabadiliko wananchi ni lazima tuwe msitari wa mbele katika kutekeleza hilo,ikiwa ni pamoja na kubana matumizi yasiyo ya lazima na kuzielekeza fedha katika shughuli za jamii,kama anavyotuonyesha mfano Rais wetu DR, J.P.Magufuli.
Kwa kweli kwa hili bado sijashawishika kama kweli tuna nia ya kuwaletea mabadiliko wananchi .Tanzania ni yetu ,wananchi ni ndugu zetu tunapaswa kujidhatiti kweli na si kufanya vitu kwa masilahi binafsi au kwa malengo ya kusaka kura zaidi hapo baada ya miaka mitano .Viongozi tuwe wazalendo wa kweli ,tuache unafiki.
By; Richard Sheim

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni