Jumatatu, 28 Novemba 2016

HUU NDIO MUONEKANO WA NDEGE INAYOMILIKIWA NA RAIS MTEULE WA MAREKANI

 
 
 
               Ikiwa ni takribani wiki tatu tangu kuisha kwa kinyang'anyiro cha uchaguzi wa marekani,ambao matokeo yake yaliiduwaza dunia  na kuacha maswali yasiyo na majibu.Ni uchaguzi ambao umeleta hisia tofauti miongoni mwa mataifa mengi ,likiwamo pia taifa la marekani. Mara baada tu ya uchaguzi yalishuhudiwa maandamano katika mitaa mbalimbali ya marekani yakipinga ushindi wa Donald Trump.Hali hiyo huenda ilichochewa na ahadi zake alizozitoa mara kadhaa katika mikutani yake ya hadhara na midahalo.Kauli zilizotawala kinywa cha Trump ni pamoja na kuwaondoa waislam,napia zile za kuwakebehi watu weusi ndani ya marekani,ila hayo yalikuwa ni maneno tu sasa tunasubiri vitendo.
                        
                 
       
           Donald Trump ni mtu tajiri na maarufu sana ndani na nje ya marekani ,umaarufu wake hasa ulikuwa na kuwa wa kidunia mara baada ya kujiingiza katika michezo hasa ya mieleka ambapo alidhamini mashindano hayo huku akionyesha mchecheto wa hali ya juu uliompelekea wakati mwingine yeye mwenyewe kuingia ulingoni na kupambana na baadhi ya wadhamini wenzie.
                
                   
                        
           Ukiacha uwekezaji katika michezo Trump pia anamali nyingine ikiwamo ndege ya binafsi amabayo huitumia kwa usafiri wake binafsi.Ndege hiyo iliyopakwa rangi nyeusi ikiwa na maandishi makubwa ya jina la mmiliki huyo (TRUMP),imeundwa kwa upekee kabisa kuweza kukidhi vigezo vyote kama matumizi ya ofisi na vingine vingi.Haina viti vingi vya kukali watu kwa maana hiyo humbeba yeye na washirika wake muhimu,ina nafasi ya kutosha sana na hairuhusu msongamano wowote ule.Ndani kuna mpangilio mzuri na pia kuna nakishi za gharama na za kuvutia Huyu ndio Trump bwana ,siku zote husema kwamba  "ASHINDANAPO HUWA HAJUI KUSHINDWA"
       

 
            By;Richard Sheim
     0653109706,
     0689699212
    
               

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni