Wana asiliasilia wenzangu ni wasaa mwingine tuna kutana tena ili tupate juzana mawili matatu kama sio manne ambayo yatakuwa na mchango mkubwa katika maisha yetu.
Watanzania tumekuwa na tamaduni moja ambayo haifurahishi kwa kweli na huenda ndo kichocheo cha sisi kutosonga mbele katika mambo mengi nayo ni ya kutotaka kujifunza mambo mapya, kama unabisha wewe sio mtu wa namna hiyo basi karibu nikuhabarishe mambo mapya yanayoendelea katika hii dunia.
Ukihudhuria sherehe nyingi hasa za harusi mara nyingi ubunifu ni uleule hasa katika upambaji wa magari yaliyoandaliwa maalumu kwa ajiri ya kuwabeba maharusi. Imezoeleka kupamba magari hayo kwa kutumia riboni na maua machache na kwa wengine huweka riboni tu.
Lakini nikaona kuna haja ya kujuzana juu ya mitindo mipya ambayo iko katika anga za kimataifa ,mitindo hiii ni ya kutumia maua kwa kuyategeneza kwa mtindo uutakao,waweza andika neno lolote kama vile la mapenzi, jina la mpenzi na kadhalika na kama haitoshi waweza chora umbo lolote alimladi tu uifanye sherehe au harusi yako itie fola.
Haya kazi kwako mwana asiliasilia mimi yangu ni hayo tu ila niendelee kukusihi uendelee kutembelea ASILI ASILI kwa mengi mazuri yanayokuja .Ubarikiwe sana
Na,Richard Sheim (0689699212)
Kwa msaada wa mtandao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni